Lagos,
Nigeria, Henry Obiefule mchekeshaji maarufu kutoka Nijeria atacheka
sana mwaka huu baada ya kupata mkataba uliompatia dola milioni 1 za Kimarekani,
(shilingi za Kitanzania zaidi ya 2,000,000,000/-). Hii ni baada ya kuteuliwa
kuwa balozi wa Vomoz Communications, au kwa Kiingereza
kuwa Brand Ambassador wa Vomoz Communication.
Obiefule
anaejulikana zaidi kama Chief Obi,
ni maarufu kwa kuigiza tabia za wazazi wa kawaida wa Kinaijeria. Historia fupi
ya Obiefule, ni kuwa alianza kutengeneza video fupi kupitia mtandao wa Keek akahamia
Vine na hatimae Instagrama alipojikuta ana followers laki mbili. Tayari
ameshashiriki katika video za muziki za 2Face, Olamide na jidenha.
Comments