Mzee Samwel John Sitta alikuwa rafiki mkubwa wa wasanii na jambo ambalo wengi hawalijui ni kuwa pia alikuwa msanii mpiga gitaa. Mwalimu wa Mzee Sitta ambaye nae ni marehemu Mzee Brown Swebe aliwahi kunambia kuwa alimfundisha gitaa Mzee Samweli Sitta wakati yuko shule ya sekondari Tabora, na alifanya hivyo kwa malipo ya kulima matuta kadhaa ya viazi. Wakati wote alikuwa kigusia umuhimu wa Hakimiliki na hata wakati akiwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba aliwezesha wasanii kukutana na wajumbe wengi wa Bunge la katiba kuweza kujielezea kuhusu umuhimu wa ulinzi wa mali isiyoshikika kutajwa katika katiba.
Tutakukumbuka daima Mzee Samwel John Sitta
Tutakukumbuka daima Mzee Samwel John Sitta
Comments