TWANGA PEPETA, NGUZA VIKING, PAPII KOCHA JUKWAANI TAMASHA LA WAFUNGWA


Bendi ya African Stars, maarufu kwa jina la Twanga Pepeta kesho itashiriki katika Tamasha la Wafungwa ambalo litaanza saa 2 asubuhi. Katika mambo ambayo yatakuwa makubwa kimuziki ni kushiriki kwa mwanamuziki mkongwe  Nguza Viking na mwanae Papii Kocha ambao kwa sasa wanatumikia kifungo cha maish katika gereza la Ukonga. Pia katika tamasha hilo atakuweko msanii nyita wa muziki wa Singeli Msaga Sumu. Lengo la tamasha hilo ni kuwatia moyo wafungwa na kuwaonyesha kuwa wapo pamoja na Watanzania wenzao walio nje ya magereza. Eric Shigongo Mkurugenzi mkuu wa Global Publishersambao ndio walioandaa tamasha amesema hii ni mara ya pili kuandaa tamasha la namna hii, ambalo lengo ni kunyanyua ari ya wafungwa. Wafungwa waliohudhuria tamasha lililopita ambao walikwisha maliza kifungo wamesifu na kusema tamasha lililopita liliwapa faraja sana. Mratibu wa tamasha hilo Juma Mbizo, amesema mbali na burudani kali kutoka kwa Twanga, kutakuwepo na michezo mbalimbali kama ya mpira wa miguu, kuvuta kamba na mingineyo ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi.  Pamoja na maneno mazuri ya kutia moyo yatakayotolewa na Eric Shigongo, Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Stephen Mwaisabila naye anatarajiwa kutoa neno katika tamasha hilo sanjari na viongozi wengine wa magereza.

Comments