KOFI OLOMIDE KUANZA KUSOTA JELA KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA DANSA WAKE


-->
Masaibu ya Koffi Olomide yamefika pabaya baada ya kuanza kifungo cha miezi 3 akisubiri uwezekano kifungo kirefu zaidi ambacho upande wa mashtaka unataka kitolewe. Adhabu hiyo ni kutokana nakosa la kumshambulia dansa wake katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International Airpot(JKIA) siku chache zilizopita. Hukumu hiyo imetolewa na mahakama moja mjini Kinshasa baada ya malalamiko kupelekwa mahakamani na Mbunge Zakarie Bababaswe, akisema amefungua malalamika kwa niaba ya umma wa Kongo. Bababaswe alifanya ‘press conference’ iliyorushwa kwenye TV akiuliza inakuwaje Kofi yuko huru wakati kuna video inayoonyesha wazi akimshambulia dansa wake. Inasemekana Mbunge huyo na Kofi zaani walikuwa marafiki wakubwa lakini waliacha urafiki huo baada ya Kofi na muimbaji wake Cindy Le Coeur, kudaiwa kuimba nyimbo za kumshushia hadhi Mbunge huyo. Kukamatwa kwa Kofi kulitokana na amri ya Mwanasheria Mkuu wan chi hiyo. Inasemekana kumekuweko na kushangiliwa kwa hatua hii nchini kongo na nje ya nchi haswa katika makundi ya wapigania haki za akina mama. Hakika hatua hii ni pigo kwa Kofi ukijumlisha kuwa umri wake si mdogo,


Comments