Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amemteua Dkt Herbert Makoye kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
Dkt Herbert Makoye |
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Mosses Nnauye amemteua Dkt Herbert Makoye kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) uteuzi
huu umefanywa chini ya Kifungu Na. 9 (1) cha Sheria ya Wakala wa Serikali,
(Executive Agencies Act) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 ambayo inampa
Waziri Mamlaka ya kufanya uteuzi huo. Uteuzi huo utaanza tarehe 01/07/2016.
Dkt Makoye amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Juma Bakari aliyestahafu
Kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma. Dkt Makoye mwenye Shahada ya Uzamivu
(PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Ghana na Shahada ya Umahiri ya Sanaa (M.A. in
Theatre Arts) toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi huu Dkt Makoye
alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Idara ya Sanaa na
Maonyesho.
Comments