KATIKA hatua ya kujua mafanikio na changamoto za muziki wa dansi na
hatimae kupanga yajayo, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
atakutana na wanamuziki wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Vijana Social
Hall Kinondoni siku ya Jumatatu kuanzia saa nne asubuhi. Hii itakuwa ni
mara ya kwanza kwa miaka mingi kwa Waziri wa Utamaduni kufanya mkutano
wa namna hii na wanamuziki.
Comments