Novemba 17, 2015, Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Airtel
leo imefungua duka jipya na la kisasa mjini Moshi lililopo katika mtaa wa
Soko Kuu. Uzinduzi wa duka hili linadhihirisha ahadi yake kwa Airtel kujali
wateja wake Tanzania nzima na kuwapa huduma iliyobora na ya kiwango cha juu
popote pale walipo.
Hii ni sehemu ya mpango wa
kampuni hiyo kuhakikisha wanatoa na kuboresha mpango wake wa huduma kwa
wateja wake ili kuongeza urahisi wa kuwafikia wateja wake mbalimbali
popote pale walipo nchi nzima.
Akizungumza katika sherehe fupi
ya ufunguzi wa duka hilo,mkurugenzi wa kitengo cha huduma za wateja wa
Airtel, Bi Adriana Lyamba, alisema kuwa ufunguzi wa duka hili jipya na la
kisasa mjini Moshi ni mwendelezo wa malengo ya Airtel kuendeleza
kuboresha maisha morani kwa kila mtanzania kwa kupata huduma zenye zenye ubora
na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote walipo.
"Tunafuraha kubwa sana
kuona tunafanikiwa kuwafikia wateja wetu na kufungua milango kwa wateja zaidi
mjini Moshi na kuwahakikishia kuwa tunafanya ubunifu wa hali
ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi
ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa
ajili ya kuwasogezea huduma karibu na wananchi, na ninawahakikishia kuwa
popote wateja wetu walipo tutawafikia , "alisema Lyamba
Duka hili jipya lenye
mazingira mazuri kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa
Airtel ikiwemo huduma za modem, Airtel Money, simu mpya za kisasa za
smartphone, huduma zetu za intanet na huduma ya malipo ya bili za awali na
mwezi .
Bi, Evelyne Zakaria ambae ni
Afisa tarafa wa Moshi Mashariki kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus
Makunga aliwashukuru Airtel kwa dhamira yake ya uboreshaji wa huduma kwa
wakazi wa mji wa Moshi. Pia alibainisha kuwa mawasiliano ni jukumu kubwa katika
kuunganisha watu na biashara ya kuendesha maendeleo katika Kata ya Moshi.
Mkuu wa Wilaya aliyaomba
makampuni mengine ya simu yajitokeze zaidi na kuiga mfano wa Airtel
katika kutoa huduma bora kwa wakazi wa mji wa Moshi akisema kuwa ofisi yake iko
tayari kwa kutoa ushirikiano kwa lengo la kufanya maisha bora kwa wakazi wake.
Comments