Uzinduzi wa Dar Kavasha Club pamoja na uzinduzi wa kitabu cha kujifunza Kilingala utafanyika leo tarehe 05-Sep-2015 kuanzia saa 12 jioni katika ukumbi wa MRC Mikocheni, ukumbi ulio nyuma ya Shopperz Plaza. Uzinduzi huo utasindikizwa na burudani kutoka kwa wana Bana Marquis bendi inayoongozwa na mwanamuziki Tshimanga Kalala Assosa, ambaye pamoja na kuwa ni kati ya wanamuziki waliokuweko katika enzi ya uanzishwaji na ukuaji wa mtindo wa Kavasha, akiwa mwanamuziki wa bendi kama Negro Success, Lipualipua, Orchestra kamale, na Orchestra Fuka fuka.
Uzinduzi huu ulikuwa ufanyike mwezi wa 5 lakini ukaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ambapo uzinduzi huo ulipangwa kufanyika.
Kiingilio cha onyesho hili ni BURE. Na hakika tukio hili ni la aina yake katika tasnia ya muziki wa dansi
Comments