KOPITAN WAANZA KUELEIMISHA WANAMUZIKI KUHUSU HAKI ZA WAANDISHI WA MUZIKI

Watunzi waandishi wa muziki wameanza kupata mafunzo toka KOPITAN kuhusu haki hii wanayostahili kupata kama sehemu ya wasanii wanaotakiwa kulindiwa haki zao na taasisi hii. Kopitan ni chombo kinacholinda haki za kazi za kimaandishi, literaly works ambazo ni pamoja na uandishi wa tungo za muziki. Hivyo wale watu wenye uwezo wa kutunga ambao huwatungia wanamuziki sasa wanaweza kulindwa na kupata mirabaha kutokana na kazi hizo. Warsha ilikosa sura maarufu za watunzi ambao walikaribishwa katika mkutano huu na kama ilivyo kawaida ya 'masuper star' hawakuhudhuria warsha hii muhimu kwa ulinzi wa kazi zao.
Mwenyekiti wa Kopitan akitoa mada
Comments