ONESHO LA TWANGA NA G5 TAARAB BALAA KUBWA

ONESHO la utambulisho wa wasanii wapya Twanga Pepeta kwa wakazi wa Temeke, lililorindima jana ndani ya Equator Grill, jijini Dar es Salaam lilionekana kukosa msisimko kutokana na kuhudhuriwa na mashabiki wachache sana. Onyesho hilo pia lilikihusisha kikundi cha G5 Modern Taarab.
Mwandishi wa habari hizi aliyekuwapo kwenye ukumbi huo ulioko maeneo ya Mtoni Kwa Azizi Ally, alishuhudia namna viti vilivyokuwa tupu kutokana na uchache huo wa mashabiki ambao hadi mwisho wa onesho idadi ya waliokata tiketi haikuzidi watu 25.
Mahudhurio hayo yasiyoridhisha kwenye onesho hilo, yalionekana kuharibu mpangilio wa ratiba ya utumbuizaji, ambapo Twanga Pepeta ilikuwa ikitumbuiza kwa muda mrefu bila kuwapisha wenzao, G5 Modern Taarab, ili kujaribu kulazimisha kuvuta wapenzi.
Mashabiki waliohudhuria onesho hilo, hawakupata bahati ya kuwashuhudia nyota wa mipasho kama vile; Abdul Misambano, Ashura Machupa na Mwanahawa Ali, kutokana na muda mchache wa kutumbuiza walioupata G5 Modern.  
Baadhi ya wanamuziki walipoulizwa juu ya hali hiyo iliyotokea jana, walielekeza lawama kwa waandaaji wa shoo hiyo, kwa kusema kuwa walizembea kwenye matangazo, huku mashabiki nao wakisema kuwa mvuto wa Twanga Pepeta umeshuka chati hivi sasa.
Wakati huohuo mcharazaji gitaa la kati, Rhythm guitar, anayekuja juu kwa kasi hivi sasa, Awadh Muhumba, ambaye ni ndugu wa Seleman Muhumba, yuko katika kipindi cha majaribio kabla hajaajiliwa na bendi African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Awadhi anayatokea kwenye bendi ya kifamilia iitwayo ‘Moro International’ inayoongozwa na ukoo wa Muhumba, ameonekana katika majukwaa ya Twanga Pepeta, kwenye maonesho yao tangu Ijumaa iliyopita, ambako ameonekana kupokewa vema na mashabiki.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Awadh alisema kuwa, anajisikia furaha kunyakuliwa na Twanga Pepeta ambapo anamini akiwa huko, atafanikiwa vilivyo kuongeza ujuzi alionao pamoja na kufahamika zaidi.
Hata hivyo, habari za chini kwa chini kutoka kwa watu walio karibu na Awadh zinasema kuwa, wazazi wa kijana huyo ambao ndio Viongozi wa bendi ya Moro International, wamemtaka asitishe uamuzi wake wa kujiunga na Twanga Pepeta ili abaki kuisaidia Morogoro International kukua zaidi...Picha za onyesho hilo hizi hapa































Comments