MPIGA GITAA AKIMBIA KUNDI LA TAARABU NA KUJIUNGA NA BENDI KUKIMBIA TUHUMA NA KUTOKA NA MKE WA BOSI

TUHUMA ya kutoka kimapenzi na mke wa bosi wake, zimemfanya mcharazaji gitaa mahiri, kulikimbia kundi la Taarab alilokuwa kilipigia na kurejea kwenye bendi aliyokuwa zamani.
Akizungumza na mwandishi wa blogu hii, mpiga gitaa huyo alisema kuwa, amechoshwa na lawama za mara kwa mara kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha Taarab  alichokuweko, akituhumiwa kumgeuka kwa mkewe.
“Kumbe kulianza kuwa na migogoro ya chini kwa chini baina yao, mke na mume, kabla ya kunikabili na kuniambia kuwa niachane na mke wake ili kuepuka kunitokea makubwa,” alisema mwanamuziki huyo ambaye pia ni mtunzi hodari anaechipukia.
Mpiga gitaa huyu anasema amerejea bendi yake ya zamani kiroho safi ambapo hivi sasa anapika kibao kikali kitakachokuwa zawadi kwa mashabiki wa bendi hiyo aliowatosa kwa kipindi kirefu.

Comments