MORO INTERNATIONAL BENDI YA WANAMUZIKI NDUGU

BENDI inayowakusanya wanandugu wengi pamoja, Moro International ya jijini Dar es Salaam, jana ilionekana kukitumia vema kiwanja chake cha nyumbani, Taxido Bar, Yombo Buza kwa kufanya shoo iliyowasisimua wengi.
Moro International inaongozwa na Marijani Muhumba pamoja na kaka yake, Shaibu Muhumba ambao ni baba wa kijana machachari katika gitaa la Solo, anayetamba na bendi ya Ruvu Stars hivi sasa, Sele Muhumba.
Katika onesho lao hilo la jana, Wana Muhumba walionekana kwenda sambamba na matakwa ya mashabiki wao kwa kumudu vema kupiga mzigo uliofaulu kukata na kumaliza kabisa kiu ya waliohudhuria.
Vibao vyao vikali pamoja na vile kadhaa vya kukopi walivyokuwa wakichanganya, vilikuwa vikichangia utamu na raha ya aina yake kwa mashabiki waliokuwa wamejazana ndani ya ukumbi huo kuwashuhudia.
Moro International hutumbuiza kwenye ukumbi huo kila wiki katika siku za Jumamosi , huku mahudhurio ya mashabiki yakionekana kuwa ni ya kuridhisha mno.Comments