MBUNGE IDD AZAN NA WAKAZI WA ILALA, KUCHEZA NA MAPACHA WATATU BURE JUMAPILI HII GARDEN ILALA

MBUNGE wa Ilala, Mussa Azan Zungu, Jumapili hii anatarajiwa kuwa mgeni kwenye Bonanza la michezo lililoandaliwa kwa ajili ya kuwakutanisha wakazi wa Ilala na kufanya mazoezi pamoja, litakalofanyika kwenye viwanja vya Garden, Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam.
Mwaandaaji wa Bonanza hilo, Vicky Don King alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, mbali ya kuwakutanisha wakazi wa Ilala na kufanya mazoezi kwa pamoja, lengo lingine la Bonanza hilo ni kudumisha undugu, urafiki pamoja na kuimarisha afya.
“Katika Bonanza hilo ambalo halitakuwa na kiingilio, kutakuwa na mechi za mpira wa miguu kuanzia majira ya asubuhi pamoja na michezo mingine mbalimbali,” alisema Vick Don King.

Alisema kuwa, kwa upande wa burudani, watakaohudhuria watapata fursa ya kufaidi uhondo wa muziki mtamu utakaoporomoshwa na bendi ya muziki wa dansi, Mapacha Watatu iliyo chini ya waimbaji Khalid Chokoraa na Jose Mara.
Mapacha Watatu ni kati ya bendi chache za kizazi kipya cha Dansi zinazofanya vizuri hivi sasa, wanaotesa na vibao vyao viwili vipya ambavyo ni ‘Sauti ya Marehemu’ na ‘Kombe Uwanjani’.

Comments