Habari zilizotufikia usiku huu 7/6/2012, ni kuwa msanii mkongwe wa Ngoma na maigizo Said Ngamba, ambaye alijulikana zaidi kwa jina la Mzee Small amefariki saa nne ya usiku katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa. Afya ya Mzee ilianza kuwa tete toka alipopata stroke. Maelezo zaidi tutawaletea kadri yatakavyokuwa yakitufikia.
Comments