Bendi ya Muziki wa dansi Ngoma Africa band alimaarufu " FFU-Ughaibuni" walipanda tena jukwaani jumamosi ya 21 Juni 2014 katika Ditzenbach Festival,nje kidogo ya mji wa Frankfurt,kule Ujerumani.
Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya yenye makao yake
nchini Ujerumani ilikuwa katika maombolezo ya siku saba kutokana na
kifo cha layekuwa Swahiba wao wa karibu bondia mkongwe hayati IRAKI HUDU
aka Kimbunga(RIP) ambaye alifariki 13.Juni 2014 mjini Dar-es-salaam.
Baada ya maombolezo hayo bendi hiyo sasa inaendelea na taratibu zake za
maonyesho huko ughaibuni.
|
JOJO SOUZA |
|
MATONDO |
|
FFU JUKWAANI |
Comments