Skip to main content

MAONI YA WACHAMBUZI KUHUSU MWENENDO WA MUZIKI WA DANSI NCHINI 2


Robbie Mwangata Asante sana kaka Sampu Mussa Sampu. Hata hivyo hapa kwetu nchini ukionekana unapenda au kuzungumzia muziki huu wa dance unaonekana kama umepitwa na wakati kitu ambacho mimi binafsi kinaniuma sana. Na kuna baadhi ya radio station hazina mpango kabisa na muziki huu. Kiuhalisia muziki huu watu wengi wanaukubali sana na kuupenda sana lakini kweli kabisa umekosa wawakilishi kila sehemu hapa nchini. Mbali na radio na Television ambazo zinawakilisha vema muziki huu lakini kuna Tv na Radio ambazo ukisikiliza wanavyouchambua muziki huu lazima utakasirika sana. kiufupi wengine hawaujui lakini wanafanya hivyohivyo kwa kuwa nadhani wamepangiwa au wenye radio na tv ni watu wao wa karibu. Kazi yangu kubwa ni udj na kwasasa utagundua kuwa hata bongo flavour na yenyewe wanataka kuwa kama dance. Maeneo mengi niliyokwenda kupiga muziki niliunganishwa na drums na kuna mtu anapiga drums kwenye kila wimbo nilioupiga. BINAFSI INANIUMA SANA.

Dakta Masomo Lupembe Genre yoyote ile ya muziki ni sawa na 'living entity' {kiumbe hai}, huzaliwa, hukua, hukomaa, huchoka, huzeeka na kisha {kama hakuna juhudi za kui-rejuvenate} inakufa! Sioni mkakati wowote wa kutaka kuunusuru muziki wa dansi; umeachwa ufe kimyakimya!


Mussa Ngayatu Fred mm nakubaliana na ww kwa asilimia 101% moja nkupa zawadi.Mm nichangie upande wa wanamuziki ambao ndio wazalishaji wakuu wa bidhaa hii.Kiukweli wao ndio wamepoteza dira na kuzalisha bidhaa hafifu ambayo haitushawishi wateja.Tatizo siku hizi kwenye band hakuna wapangaji wa muziki ila tu mwenye sauti ndio hupanga muziki!Matokeo yake yy mwenyewe hajui kisha huyo huyo ndio apangie wengine!Utunzi,hapa ndio kwenye tatizo kila mtu ni mtunzi!Zamani kulikuwa na watunzi tena wengine hawjishughulishi kabisa na muziki lkn band/wanamuziki walitungiwa nyimbo na wao kuziimba tu.Lkn siku hizi ukiwa mwimbaji basi tayari una cheo cha kutunga!Matokeo yke mtu anajitungia tu!Kibaya zaidi hakuna wahariri wa hizo nyimbo!Tuna ushahidi wa nyimbo ambazo zilitungwa na watu wasiojulikana na zilibamba.Band zibadilike zifuate misingi na sheria za muziki

Comments

Popular posts from this blog

Unataka kujifunza muziki?

Je ungependa kujua Kurekodi muziki, Kusoma Muziki, Kuandika Muziki, Kuimba na Kupiga Ala mbalimbali za kisasa za muziki ? Kama ndivyo, basi waone AlphaBeta Music Centre waliopo TABATA Liwiti mkabala na shule ya msingi au wasiliana nao kwa simu +255 754 77 66 40 au +255 784 737 216. Usiikose fursa hii!!!!!

TWANGA PEPETA, NGUZA VIKING, PAPII KOCHA JUKWAANI TAMASHA LA WAFUNGWA

Bendi ya African Stars, maarufu kwa jina la Twanga Pepeta kesho itashiriki katika Tamasha la Wafungwa ambalo litaanza saa 2 asubuhi. Katika mambo ambayo yatakuwa makubwa kimuziki ni kushiriki kwa mwanamuziki mkongweNguza Viking na mwanae Papii Kocha ambao kwa sasa wanatumikia kifungo cha maish katika gereza la Ukonga. Pia katika tamasha hilo atakuweko msanii nyita wa muziki wa Singeli Msaga Sumu. Lengo la tamasha hilo ni kuwatia moyo wafungwa na kuwaonyesha kuwa wapo pamoja na Watanzania wenzao walio nje ya magereza. Eric Shigongo Mkurugenzi mkuu wa Global Publishersambao ndio walioandaa tamasha amesema hii ni mara ya pili kuandaa tamasha la namna hii, ambalo lengo ni kunyanyua ari ya wafungwa. Wafungwa waliohudhuria tamasha lililopita ambao walikwisha maliza kifungo wamesifu na kusema tamasha lililopita liliwapa faraja sana. Mratibu wa tamasha hilo Juma Mbizo, amesema mbali na burudani kali kutoka kwa Twanga, kutakuwepo na michezo mbalimbali kama ya mpira wa miguu, kuvuta kamba na mi…

RATIBA YA MSIBA WA MAREHEMU SALOME KIWAYA

Taarifa ya ratiba ya msiba wa marehemu Salome Kiwaya aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma na mwanamuziki, aliyefariki jana 07/10/2016, kwa ajali ya gari maeneo ya Kilimo Kwanza Dodoma Mjini. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Image, Kata ya Kilimani, Wilaya ya Dodoma Mjini. RATIBA:
1.Tarehe 08/10/2016 - maombolezo  yanaendelea nyumbani Image Kilimani Dodoma.
2.Tarehe 09/10/2016 kuanzia saa 2:00 asubuhi - mwili wa marehemu utaletwa nyumbani kutokachumba cha maiti cha General Hospital Dodoma.
3. Tarehe 09/10/2016 saa kuanzia 6:00 mchana -salamu mbalimbali za Viongozi na Makundi Maalumu zitaanza kutolewa.
Saa 8: 00 mchana- mwili wa marehemu utatolewa nyumbani, na kuelekea Kanisa Kuu Roman Catholic. Baada ya Misa, msafara wa mwili wa marehemu utaelekea Kijiji cha Mtila, Kata ya Matola Mkoa wa Njombe kwa ajili ya maziko tarehe 10/10/2016 siku ya Jumatatu.