TANZANIA MUSICIANS NETWORK wakishirikiana na BASATA watafanya warsha ya kwanza ya siku moja kwa viongozi wa bendi na vikundi vingine vya muziki, Warsha hii itakuwa ya kwanza katika warsha za kubadili mwelekeo wa maendeleo ya muziki wa bendi Tanzania. Warsha hii itafanyika katika Ukumbi wa Basata siku ya Jumanne tarehe 25 March kuanzia saa nne asubuhi. Viongozi wa bendi mbalimbali karibuni
Comments