Mkutano wa kwanza wa viongozi wa bendi mwaka huu, uliofanyika katika
ukumbi wa Basata Jumanne tarehe 25 March umekuwa na mengi mazuri. Kwanza wanamuziki
walikumbushwa mengi ambayo yameshindikana kufanyika kwa kutokuweko na umoja
wenye nguvu wa wanamuziki, hasa wa muziki ‘live’, hivyo kulipatikana azimio
kuwa wanamuziki wahamasishane wenyewe kujiunga na vyama vya muziki.
Maelezo pia
yalitolewa kuhusu nafasi ya sanaa katika Katiba mpya na juhudi ambazo
zimekwisha fanywa na jinsi zinavyohitaji umoja katika kipindi hiki cha Bunge la
Katiba. Viongozi hawa hatimae walizungumzia changamoto mbalimbali ambazo
zinaikumba tasnia hii, na kuamua kuanza kujipanga kupunguza matatizo yale
ambayo yako katika uwezo wa bendi. Iliamuliwa kuweko na kikao kingine Jumanne
ijayo kuanzia saa nne asubuhi palepale BASATA na kutafuta wajumbe wengine kutoka bendi ambazo hazikuhudhuria mkutano wa leo.
Comments