Skip to main content
BABU NJENJE ARUDI JUKWAANI BAADA YA KUUGUA KUANZIA 9 DESEMBA 2013
BABU
NJENJE, kwa jina halisi Mabrouk Khamis, jana Jumamosi tarehe 8 March
2014 alipanda tena jukwaani na kushirikiana na bendi yake Kilimanjaro
Band aliimba nyimbo kadhaa ambazo zinapendwa na wapenzi wa bendi hiyo.
Babu Njenje alipata stroke tarehe 9 December 2013 wakati akijitayarisha
kwenda kwenye onyesho la bendi hiyo lililokuwa lifanyike katika ukumbi
wa Escape One kusherehekea siku ya Uhuru. Katika kupata stroke hiyo
aliathirika mguu na mkono wa kushoto. Taratibu katika kipindi hiki
amekuwa anapewa matibabu na hatimae jana akafika jukwaani na kuimba
nyimbo zake. Pamoja na kuwa bado anaendelea na matibabu kwa bado hawezi
kusimama na anahitaji wheelchair kusafiri, lakini Mungu ni wa
kushukuriwa hadi hapa alipofika. Kwa taarifa yake mwenyewe aliwashukuru
wapenzi wa Njenje na kumtaja haswa BI Salma Mtambo kwa kumwezesha
kufikia hali hiyo ya afya.
Comments