SHIRIKISHO LA FILAMU (TAFF) WAKABIDHI MAPENDEKEZO YA SERA YA FILAMU

SHIRIKISHO LA FILAMU (TAFF) Jana Jumatatu limekabidhi utafiti wake ambao ndani yake kuna mapendekezo ya ya sera ya Filamu kwa Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo. Shughuli hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa vyama mbalimbali vinavyohusiana na filamu kama vile Chama cha waongozaji wa Filamu, Chama cha waandishi wa Script, Chama cha Waigizaji, Chama cha Wasambazaji na vinginevyo vya aina hiyo. TAFF iliongozwa na Rais wake Simon Mwakifwamba
Comments