MKUTANO WA WASANII NA VYOMBO VYA HABARI WAFANYIKA

MKUTANO ULIOKUSANYA WASANII WA FANI MBALIMBALI ULIFANYIKA LEO KATIKA UKUMBI WA VIJANA KINONDONI AMBAPO MGENI RASMI ALIKUWA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BASATA. MKUTANO HUO AMBAO ULIHUDHURIWA NA WAANDISHI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI ULIFANA KWA AINA YA MACHANGANYIKO WA WASANII. WASANII WALIKUWA HAPO KUELEZA AZMA YAO YA KUONA SWALA LA WAO KUTAMBULIKA KATIKA KATIBA LINASHUGHULIKIWA NA SWALA LA MILIKIBUNIFU (INTELLECTUAL PROPERTY) LINAWEKWA KATIKA KATIBA. BAADA YA MKUTANO NA WAANDISHI WASANII WALIBAKI NA KUTAFAKARI TUNAKOELEKEA NA PAMOJA NA MENGINE ILIPENDEKEZWA KUFANYIKE MAANDAMANO YA KUSHUKURU KUPATA MUWAKILISHI KUTOKA KUNDI LA WASANII
Comments