Jokate Mwegelo mgeni rasmi katika kuzindua awamu ya tisa ya wanafunzi wa TFTC

Kile kituo maarufu katika kufundisha mbinu mbalimbali za utengenezaji wa filamu, TFTC, leo kimefungua ukurasa wa awamu ya tisa ya darasa hili toka kundi la kwanza lianze. Hakika kituo hiki kinachoendeshwa na Pastor Myamba kinahitaji pongezi kwa kazi nzuri kinachofanya katika kuendeleza sekta ya filamu Tanzania. Mgeni rasmi siku hii ya leo alikuwa Jokate Mwegelo ambaye licha ya kutoa hotuba nzuri ya kujenga pia alitoa vita kwa ajili ya kuendeleza maktaba ya kituo. Wageni wengine waliokuweko walikuwa Simon Mwakifwamba Rais wa Shirikisho la Filamu, Steve Nyerere mwenyekiti wa Bongo movie Unit, John Kitime Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki, Kajala msanii maarufu wa filamu.
Wasanii wakituo walionyesha vipaji vingi vikiwemo uigizaji, uimbaji na uchekeshaji

Comments