UBALOZI WA MAREKANI WATOA VITABU VYA HAKIMILIKI KWA AJILI YA WASANII TANZANIA

Afisa wa Ubalozi wa marekani akimkabidhi John Kitime(Mwenyekiti) na Abraham Kapinga( Katibu Mkuu) vitabu 800 vya elimu ya haki za wasanii
Ubalozi wa marekani nchini Tanzania, leo hii 7/11/2013 umemkabidhi  vitabu vya Hakimiliki zaidi ya 800 Mwenyekiti wa Tanzania Musicians Network, John F Kitime katika hafla iliyofanyika katika maktaba ya Ubalozi huo uliopo jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho chenye lugha mbili Kiswahili na Kiingereza kimetungwa na  Alex Perullo ambaye ni Associate Professor wa Anthropology na African Studieskatika chuo cha Bryant Marekani. Hiki ni kitabu cha pili cha aina hii kutungwa na Profesa huyu, cha kwanza alikisambaza kupitia Ubalozi huu huu miaka kumi iliyopita. Kwa vile kina lugha mbili kitabu hiki kina majina mawili kinaitwa Artistic Rights na Haki za Kisanii. Ni kitabu cha kurasa 98 ambacho kimejaa maelezo mengi kuhusu haki za wasanii, wasanii watakao kisoma watafaidika sana.Mtandao wa Muziki Tanzania, utakisambaza kitabu hiki katika taasisi mbalimbali muhimu na pia utawapa bure wanachama wake nakala za kitabu hiki muhimu. Dibaji ya kitabu hiki imeandikwa na John Kitime.Comments