NDEGE WATATU, KUNDI JIPYA LA WANAMUZIKI WA KIKE WANAOUJUWA MUZIKI-WASIKILIZE KWA MARA YA KWANZA HAPA

Pauline Zongo, Khadija Mnoga, Joan Matovolwa
Mabinti watatu waimbaji maarufu wameungana na kutengeneza kundi jipya na kujiita NDEGE WATATU, wametoa wimbo mtamu sana ambao umenogeshwa zaidi na uwezo wao wa hali ya juu wa kuuimba katika lugha tofauti tatu, Kiswahili, Kilingala na Kiingereza. Hao si wengine ni Khadija Mnoga ambaye kwa sasa yuko Extra Bongo lakini ana ujuzi wa muda mrefu kwa kupitia bendi kadhaa, Joan Matovola ambaye alivuma katika muziki katika kibao alichokifanya na Dataz miaka kadhaa iliyopita, kilichoitwa Mume wa mtu. Baada ya hapo amekuwa kitumia muda mwingi katika sanaa ya uigizaji katika filamu. Pauline Zongo, binti wa Kikongo aliyeingia nchini akiwa na mpiga gitaa wa kundi la wanawake watupu ambalo bahati mbaya halikudumu sana, na ambaye kundi lake la mwisho lilikuwa TOT naye yumo katika kundi hili akipiga gitaa na kuimba pia. Waimbaji hawa wamekaa pamoja na kuja na wimbo waliouita Misukosuko.

Comments

Anonymous said…
Very nice song,very nice combination,very nice voices!!