Mwanamuziki Chiwoniso Maraile wa Zimbabwe amefariki dunia baada ya
kuugua kwa matatizo ya mapafu. Chiwoniso ambaye amewahi kuja Tanzania na
kurekodi katika studio za Marimba Studio akifanya kazi na wanamuziki wa
hapa nchini kama Karola Kinasha, Norma Bikaka, Bob Rudalachini ya Producer toka Norway Sigbjorn Nedland, alikuwa
mahiri sana kwa chombo chake cha Mbira na kuimba pia. Chiwoniso akiwa na Karola Kinasha na wenzao wengine toka Ethiopia, Norway, na mmoja wa wanamuziki wa Zapp Mama toka Ubelgiji, walikuwa katika kundi la bendi ya wanawake watupu walioweza kuzunguka sehemu nyingi duniani na kundi lao walililiita Women with Voices.
Wimbo wake mmoja hupiga kama signal tune ya kipindi cha akina mama kila Jumamosi Radio One Mungu amlaze pema mwenzetu
Wimbo wake mmoja hupiga kama signal tune ya kipindi cha akina mama kila Jumamosi Radio One Mungu amlaze pema mwenzetu
Comments