Msanii mwingine wa Hiphop Langa Kilewo ayelianza kujulikana
katika kundi la Wakilisha akiwa na Witness na Shaa amefariki dunia mchana huu.
Taarifa za Langa kuwa amelazwa hospitali zilianza kujulikana mapema leo katika
blog kadhaa zenye kufuatilia wasanii, zikieleza kuwa kalazwa kwa tatizo la malaria. Langa ambae aliwahi kukiri hadharani kuwa
ana tatizo kubwa la madawa ya kulevya na kutangaza kuwa ameachana na madawa
hayo kutokana na matatizo yaliyokuwa yanamletea. Hivi karibuni kama wiki mbili zilizopita, Langa
alikuwa akihojiwa katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV akawa akimuongelea marehemu Ngwear na kumsifu
sana kuwa alikuwa na roho safi, pia Langa alikuwa anaelezea mipango yake ya baadae baada ya
kutoa video yake mpya aliyoifanya na P Funk na Fid Q iliyokuwa ikiitwa Rafiki
wa kweli. Alikuwa akiongelea kukamilisha video zake nyingine mbili ili kutoa
album mwishoni mwa mwaka. Hayatakuwa.
MUNGU AMLAZE LANGA KILEWO PEMA PEPONI
Comments