ALBERTH KENNETH MANGWAIR...HITIMISHO

Hatimae mwili wa Mangair umewasili jana kutoka Afrika ya Kusini ambapo alikumbwa na kifo cha ghafla akiwa katika hatua za mwisho za kurudi nyumbani baada ya kufanya maonyesho nchini humo.
Albert  Kenneth Mangwea alizaliwa Mbeya tarehe 16 November mwaka 1983 akiwa ni mtoto wa mwisho kwa baba yake aliyekuwa na watoto 10, na mtoto wa 6 kwa mama yake. Mapema familia yake ilihamia Morogoro ambapo akajiunga na shule ya msingi Bungo hadi Darasa la 5 kisha akahamia Dodoma pamoja na baba yake nakumaliza elimu ya msingi katika shule ya Msingi Mlimwa Dodoma.Alijiunga na shule ya sekondari ,na  huko ndiko alikutana na wasanii wenzie akina Mez B, Noorah na wengine na kuanza harakati za sanaa yake.

Alikuja Dar es Salaam na mwaka 2003 na chini ya P Funk wa Bongo Records alirekodi kibao kilichomtambulisha rasmi kilichojulikana kama Gheto Langu na jina la Ngwair likawa rasmi hewani. Ngwair alitoa album yake ya kwanza 2004 iliyojulikana kama AKA MIMI, album iliyopata tuzo la Kilimanjaro Music Awards ikiwa ni  album bora ya Hiphop , pia album hiyo ilikuwa na wimbo Mikasi uliyoleta malumbano katika jamii hata kutajwa na BASATA kuwa upigwe marufuku.
 Album yake ya pili iliitwa Nge iliyotoka 2009, ikawa na nyimbo kama CNN na Nipe Dili ambao ulimpatia tuzo lnyingine ya Kilimanjaro Music Awards ukiwa wimbo bora wa Hiphop.


Leo mwili wake utaagwa katika viwanja vya Leaders Club na baadae kuelekea Morogoro kwa mazishi.
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMEN

Comments