SHIWATA YAZINDUA MAONYESHO YA BURE YA SANAA YA KILA MWEZI

Shirikisho la Wasanii Tanzania katika kitendo kinachotakiwa kuungwa mkono na wadau wote wa sanaa kimeanzisha taratibu ya kufanya maonyesho ya bure kwa wasanii wote ambao bado hawajaweza 'kutoka'. Maonyesho haya yatafanyika kila mwezi, safari hii maonyesho yalianza katika ukumbi wa Starlight Dar es Salaam. Zaidi ya wasanii mia moja walishiriki, wakionyesha vipaji vyao katika nyanja mbalimbali za sanaa. Kilichosikitisha ni jitahada za Afisa Utamaduni mmoja kujitahidi kwa uwezo wake wote kuzuia onyesho hili, ambapo akili ya kawaida inaonyesha kuwa yeye angekuwa mdau wa kwanza kutafuta kila njia shughuli hiyo ifanikiwe.
Dancers

WatazamajiMichoro

Matarumbeta

TaarabMduara
Comments