LADY JD ATOA WOSIA... RUGE MTAHABA NA JOSEPH KUSAGA WASIHUDHURIE MSIBA WAKE

Katika hali ambayo haijawahi kutokea katika tasnia ya muziki kwa kumbukumbu zangu za miaka zaidi ya 30 ambayo nimekuwa mwanamuziki  MWANAMUZIKI LADYJD AMETOA MATAMKO MAZITO SANA KATIKA BLOG YAKE. Pamoja na mengine mengi ametamka maneno ambayo huchukuliwa kwa uzito sana katika jamii ya Kiafrika, nanukuu…… Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu….. haya ndiyo yote aliyoandika……….

 
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu

JIDE

Comments

DADA JIDE HUO NDIO USANII, KWA KUWA MUNGU NDIYE NGAO KWA WAMKIMBILIAO NA WATENDA HAKI BASI ITABAKIA HIVYO NA KILA MTU NA RIZIKI YAKE- NIMESHUHUDIA SKYLIGHT BAND WANALAZIMISHA IJULIKANE LAKINI WAPI!!!!!!! KABLA YA KUANZA KUSEMA NILIVYOONA WAIMBAJI WAKO JONICO NA MWINYI WAMEHAMIA SKY NIKAJUA TU KUNA MKONO WA MTU. ACHA WAENDELEE NA ROHO ZAO MBAYA NA DAIMA ZITAENDELEA KUWA MBAYA KWANI BIBLIA INASEMA: "NA MWENYE UCHAFU NA AENDELEE KUWA MCHAFU". NA JK NYERERE ALISEMA:"MTU AKIANZA KULA NYAMA YA MTU KAMWE HATAACHA."
salim seif said…
Kaza hapohapo. Wakongwe twasema kua uyaone. Wape methali hii : MUNGU HAKUPI NGUVU NA MBIO, UTAUA WENZIO.muhozi bunura said…
pole sana mdogo wangu kwa hayo unayopitia mungu wetu ni mwema atakupigania utashinda soma KUTOKA 14:14
Anonymous said…
Mh! Pole sana dada, inaonekana hawa jamaa wanajisahau sana.....lakini kama unavyoani, iko siko utafanikiwa zaidi yao, riziki ya mtu haizuiriwi, inacheleweshwa tu!
Lawrence Ambrose said…
Pole sana Dada Jay_D na usiwaze wala usiwasikilize hao, maana mtu akitenda lililo BAYA wewe tenda lililo ZURI, mfano kama ulivyoamua kusema UKWELI hiyo safi sana!, hatima yake Aibu na watajidharau. Songa mbele mdada...
Anonymous said…
Nakukubali KAMANDA....watashindana lakini hawata shinda.....Roho zao Nyeusi hata Shetani Anawaogopa....
Tutatekeleza wosia wako.

dede
Anonymous said…
Hawa clouds na jopo lote hilo la akina Kusaga,Ruge nk.wamezidi sana ku dominate ktk tasnia hii ya sanaa,hii inawapa vichwa kunyanyasa wasanii kwa kadri wawezavyo,mambo haya yamekuwa yakisemwa lakini naona wizara husika hajayatilia maanani,Nakumbuka hata MR.Two aliwahi kuwapa ukweli wao lakini hakuweza kuungwa mkono na watu,Mimi naamini ayasemayo Jide hawa watu(Clouds)wamezidi sana kuwa na tamaa na pia kivihujumu vukundi vingi vya sanaa,Naamini hata kuzorota kwa muziki wa dansi Tanzania hii redio ya Clouds imechangia kiasi kikubwa.Cha msingi hapa ni kuiomba wizara husika km Utamaduni na pia wizara ya habari kuweza kuwaonya majitu haya yaliyojaa tamaa na roho mbaya,Mwisho wao utafika tu,hakluna lisilo na mwisho.Mwanamuziki mkongwe Ugaibuni.