Wiki hii imekuwa mbaya sana kwa muziki wa Taarab. Katika wiki hii, Haji Mohamed
Mkurugenzi wa East African Melody, kundi lililoanzia Zanzibar na kufikia
kutikisa nchi za Afrika Mashariki, Kati na hata Uarabuni, alifariki kwa maradhi
katika hospitali ya Muhimbili. Leo hii tumempoteza Bibi kipenzi Bi Kidude. Bwana
Haji ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga kinanda chenye
|
BI KIDUDE |
|
HAJI MOHAMED |
scale za kizungu
na kupiga kinanda kilichokuwa katika scale za Kiarabu, pia alikuwa muimbaji
mahiri wa nyimbo za Kiswahili na Kiarabu. Na aliwahi kusema Bi Kidude alikuwa
mmoja wa waalimu wake. Bi Kidude ambaye alikuwa akiweza kuimba Kiswahili na
Kiarabu pia alikuwa mahiri aliyesema kuwa alikuwa anafuata nyayo za Siti Binti
Sadi. Wawili hao mtu na mwanafunzi wake wametuacha wiki hii.
Mungu awalaze pema
peponi
Comments