KILI MUSIC AWARDS 2013 -KIKWETUKWETU KWELI?


Mwanamuziki mkongwe na sound engineer wa miaka mingi, ambaye amekwisha fanya kazi hiyo ya kurekibisha sauti katika matamasha chungu nzima hapa nchini yakiwemo BUSATA NA ZIFF, na pia kufanya kazi hiyo hata katika matamasha nchini NORWAY bwana Keppy Kiombile ameandika haya katika ukuta wake kwenye Facebook
Tuwe wakweli pale tunapo zungumzia ukweli inatangazwa na ndivyo itakavyokua KILIMANJARO MUSIC AWARD 2013 inakuja kwa slogan ya "KIKWETUKWETU" maana yake ni nzuri sana kwa wasanii washiriki wa Kitanzania, na wahusika wahudumiaji ki "logistic"  wa uendeshaji shughuli Watanzania. Ila ninachokiona na kukipinga ni ukweli kuwa itakapo fika wakati fungu la pesa za uendeshaji shughuli hizo kutoka, wataalam ndani ya oganaizashen wanapeleka mahela nchi jirani na kuleta waendeshaji kwa kusema wana vifaa bora, na wanajua kuliko waendeshaji wa hapa. Hapana ukweli ila hasahasa hizo ni njama za kula pesa tu, je, kampuni na taasisi za Kikwetukwetu hata kama mnaziona hazijui kuaandaa zitajua lini kwa mfumo unaoendelea? hii ndio nafasi yao ya kujifunza kama hazijifunzi na cha nyumbani ziende wapi? Ukweli hizo hizo kampuni za kigeni zinapokuja, wanakuja watupu wanakodisha vifaa hapahapa bongo bila nyie kujua. Je, mnajua mnachokifanya? Mna fikira za Kikwetukwetu kweli? wasanii waligoma mcpeleke hela kwa mastaa wa nje kwani hii ni shughuli yao wapeni hela zote wenyewe wapige show mmewasikia basi fanyeni kila kitu Kikwetukwetu kweli. ni mtazamo zaidi "bias"............
Haya changamoto kwa watayarishaji, vifaa tunavyo, watu wapo, kwa kuwa kazi zinazoshindaniwa zimerekodiwa Kikwetukwetu, hicho kipengele cha logistic vipi???????????

Comments