Sunday, March 24, 2013

MATAYARISHO YA SENDOFF YA SUSAN LEWIS aka NATASHA

Msanii maarufu mwenye heshima nyingi Tanzania, Mama Mona au maarufu Natasha leo amaenza vikao vya Natasha's Nite au sendoff kuelekea kwenye harusi yake. Sendoff imepangwa kuwa mwishoni mwa mwezi May. Ndugu na marafiki wa Natasha na wasanii mbalimbali kutoka sura mbalimbali za sanaa ikiwemo muziki walikusanyika kujaribu kukusanya fedha za kuwezesha kufanikisha siku hiyo. Kikao kikiongozwa na MC mahiri ambaye pia ndie Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba kiliweza kukusanya robo ya matarajio ya mchango katika siku hii peke yake. Blog hii inamtakia Natasha mipango murua na kuwezesha kufanikisha ndoto yake.

1 comment:

Anonymous said...

Hongera zake anastahili kua mke

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...