KILI MUSIC AWARDS 2013 ZAZINDULIWA KWA KISHINDO
Baraza la sanaa la Taifa, BASATA na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo wamezindua rasmi tuzo za muziki za Tanzania zijulikanazo zaidi kama Kili Music Awards kwa mwaka 2013 kwa kusaini makubaliano ya TBL kuendelea kufanya mchakato huo kwa miaka mitano ijayo. Sherehe ya kutoa tuzo hizi mwaka huu zitakuwa pale Mlimani City tarehe 8 mwezi June 2013. Kauli mbiu ya Awards za mwaka huu ni Kikwetukwetu zaidi katika kuonyesha kuwa tuzo hizi ni za nyumbani kwa watu wetu muziki wa nyumbani ukifanywa na wasanii wa nyumbani.
Bia ya Kilimanjaro kwa kudhaminituzo hizi kwa miaka mitano ijayo itatumia zaidi ya shilingi bilioni 4 kwa maandalizi.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alikumbusha maneno haya “Wale wanaofuatilia tuzo za muziki Tanzania, barani Afrika na duniani kwa ujumla mtakubaliana na mimi kabisa kwamba tuzo hizi kwa hapa Tanzania na kwa Afrika kwa ujumla ni za ukubwa kuliko tuzo zote zinazotolewa, ilikuwa inatanguliwa na Kora Music, MTV na Channel O awards.”

Comments