LADY JD NA JOTO HASIRA KILA KONA YA NCHI


Joto Hasira wimbo mpya wa Lady JD akiwa amemshirikisha  Professor Jay, umesambaa karibu nchi nzima kutokana na hali iliyopo sasa ambapo nyimbo mpya huwekwa katika mitandao kwa mfumo wa free download, hiyo huwezesha mtu kupata wimbo huo bure na kinachofuata ni wafanya biashara kudown load na kuanza kuuza kwa kuchoma CD au kuhamishia kwenye Flash. Kwa kuwa Bodaboda nyingi zinatumia mtindo wa kutumia flash, rafiki yangu kutoka Rombo alifanya uchunguzi na kunambia karibu kila Bodaboda huko wimbo ina wimbo huo, yamkini hali hiyo ndio ilivyo kwa Bodaboda nchi nzima.
Kama hujausikia wimbo huu ambapo JayDee na Prof Jay kila mmoja amewakilisha kipaji chake vyema. Japo ningefurahi zaidi kungekuweko na ubunifu zaidi katika mpangilio wa vyombo.


Comments