The Rwanda Movie Awards
zilizofanyika Kigali Serena Hotel siku ya Jumapili iliyopita zilikuwa ni
shughuli ya masaa matatu na nusu yenye shamra shamra za hali ya juu, zilizoongozwa na
mtangazaji maarufu wa Radio Rwanda Tidjara Kabendera.
Irene Uwoya akiwakilisha |
Shughuli nzima ilianza saa
moja kamili usiku ambapo wapenzi wa filamu toka kila kona ya jiji la Kigali
waliingia katika ukumbi wa Serena Hotel ili kuona kuzinduliwa kwa Rwanda Movie
Awards. Nyota wa filamu kutoka Tanzania walikuwepo wakiwakilishwa na Irene
Pankras Uwoya, Ray Kigosi na Jacobs Stephen, walioambatana na mchekeshaji
maarufu King Majuto
King Majuto akiingia ukumbini |
Tuzo zilitolewa kwa category
mbalimbali ambazo zilifuata maamuzi ya majaji, na pia kulikuwa na kura kupitia
internet ambazo zilizotoa ‘people's choice’. Kulikuweko na category kumi ikiwemo
ya the Best Child actor. Tuzo zilikwenda kwa wafuatao;
Best film documentary: The
impact of given a cow to the people of Rwanda by Ishmael Ntihabose.
Best short film: Kivuto
Best Actor: Munanura
Habyalare
Best Actress: Fidelite
Irakoze Sonia
Best Director: Muniru
Habyakare
Up coming group/Dynamic
awards: Happiness Games
People's Choice Actor: Denis
Nsanzabaganwa
Best Female People's Choice:
Marie France Niragire.
Best People's Movie: Ibanga
Young Best Actress: Esther
Ngabire
Kikundi cha Bibaho Film Actors, ndio kilichukua tuzo ya Best
Actors' kwa mwaka 2012-2013. Mkurugenzi wa kundi hili Muniru Habyakare
alichukua tuzo la Best Director na Best Film Actor of the year
Mmoja wa majaji Kennedy Mazimpaka, akielezea kwanini
ililazimika kuweko na majaji alisema katika kuchambua filamu ililazimika
kuchambua kitaalamu script, kuangalia ubora wa sauti katika filamu na hata
jinsi waigizaji walivyotimiza kazi yao, ila mambo mengine yalitegemea kura za
wapenzi kupitia internet. Uwepo wa wasanii wetu wa Tanzania katika shughuli
hiyo hakika ni ushahidi wa hatua kubwa waliyofikia katika tasnia ya filamu Afrika Mashariki
Comments