TAARIFA NZURI NA MUHIMU kwa wanamuziki na ma
Producer, na wenye label za muziki Tanzania, hususan Dar es Salaam.Mkurugenzi mtendaji CEO
wa kampuni ya Africori, kampuni ambayo husambaza kazi kwa kupitia mitandao,(online
digital distribution company) atakuweko hapa nchini kukutana na wale wenye nia
ya kusambaziwa kazi zao kwa kutumia njia hiyo, ambayo itaweka muziki(audio na
video) katika mtandao na kuweza kununuliwa na watu wote ulimwenguni na pia hata kuonekana na makampuni ya kimataifa yenye uwezo wa ununuzi wa haki
za muziki wa kwenye simu(ringtones), na kukuachia asilimia kubwa ya mauzo hayo. Kwa wale
wenye nia ya kuonana na mfanyabiashara huyu, atafika nchini Jumanne tarehe 12
March na kuondoka Alhamisi tarehe 14, wenye nia ya kuonana nae na wenye kazi za
kuuza tafadhali nitaarifuni kupitia email jkitime@gmail.com
Comments