Saturday, February 23, 2013

WARSHA YA WAPIGA BASS YAFANA

Hatimae ile warsha ya wapiga bass guitar iliyokuwa ikiendeshwa na mpiga bass mahiri kutoka Marekani Tony Bunn na  iliyochukua siku 3 imekwisha jana Ijumaa ikifuatiwa na onyesho la masaa matatu ya upigaji mbalimbali wa wapiga bezi, mara nyingine kukikwa na wapiga bezi wawili katika wimbo mmoja wakifanya yale waliyojifunza. Kikubwa kilichoonekana wazi ni kuwa tuna wapiga bezi mahiri sana wenye uwezo wa kimataifa, swali ni kwanini hawa huwakuti kwenye bendi zetu tunazozifahamu?Warsha hii ilitayarishwa na Eyecuemedia na Tanzania Musicians Network. Nyingine zinakuja.

Tony Dunn mwenye kofiaMzungu Kichaa

John Kagaruki wa Eyecuemedia


No comments:

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...