MSHIRIKI WA BIG BROTHER AFRICA GOLDIE AFARIKI DUNIA


Msanii Goldie Harvey  ambaye jina lake halisi ni Susan Oluwabimpe Harvey, aliyezaliwa 23 Oktoba 1983, amefariki ghafla katika hospital ya Reddington Victoria Island Lagos , muda mfupi baada ya kutoka Marekani. Bado chanzo cha kifo chake hakijajulikana. Goldie aliyekuwa chotara wa Kinaijeria na Kiingereza alikuja kujulikana zaidi Afrika Mashariki kutokana na kushiriki kwake katika shindano la Big Brother Africa na kuwa na ukaribu sana na msanii wa Kenya Prezzoo, kiasi cha kupachikwa cheo cha 'shemeji' na wapenzi wa shindano hilo wa huku. Goldie alikuwa mwanamuziki alieanza safari yake ya muziki 2006, alipotoa album yake iliyoitwa ‘Spin me’ iliyokuwa na nyimbo nne zikiwemo, Komole, Nothing has changed, Shift, na Spin Me. Kwa wakati huu ana single mbili ambazo ziko kwenye top charts za Nigeria ambazo ni You know it na DJ play on.
Mungu amlaze Pema peponi

Comments