Mchekeshaji wa kike maarufu Tumaini Martin, maarufu kwa jina la Matumaini ameweza kurudishwa nchini juzi kwa jitihada za wadau wa sanaa na wasanii wa uigizaji wenzie. Matumaini aliyekwenda kutafuta maisha nchini Msumbiji mwaka mmoja na nusu uliopita alikumbwa na matatizo ya afya na kuwa katika hali mbaya iliyolazimisha achangiwe na wenzie ili kurudi nchini. Jambo la kufurahisha ni kuwa baada ya kurudi nchini na kulazwa hospitali kwa siku moja tu ameweza kupata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwa wazazi wake . Blog inamtakia heri ya kupona kwa haraka
Comments