Monday, January 7, 2013

Mwanamuziki Omary Omary afariki dunia

Wimbi la wasanii vijana kufariki limepiga tena hodi. Msanii wa muziki wa mchiriku Omary Omary amefariki dunia. Msanii huyu ambaye taarifa zinasema alikuwa kalazwa kwa kipindi katika hospitali ya Temeke, alipata unafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani lakini akazidiwa tena na kurudishwa hospitalini hapo, ambapo usiku wa kuamkia leo akakata roho. Msiba wa Omary Omary upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini. 
MUNGU AMLAZE PEMA AMEN

No comments:

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...