ZUKU SASA KUWEZA KULIPIWA KUPITIA MAXCOM

Meneja Mkuu wa Zuku Fadhili Mwasyeba akiongea, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa MaxMalipo Ahmed Lussasi

Kampuni ya ZUKU Pay Tv imeingia mkataba na kampuni ya MAXMALIPO ambao utawarahisishia sana wateja wa ZUKU kuweza kulipia matumizi ya ZUKU kupitia mashine za Maxcom ambazo zimezagaa sehemu nyingi sana nchini. Wateja sasa wakiwa na Zuku Subscription ID wataweza kuchagua kulipia kati ya huduma kadhaa ambazo ZUKU inazo kama vile Zuku Classic, Zuku Premium, Asia Classic, au Asia Premium. ZUKU inastesheni za Burudani, Habari na sinema kama vile BBC, MTV BASE,Sentanta Sports, MGM Movies na nyinginezo nyingi. Huduma  ya ZUKU hupatikana Tanzania nzima kupitia satelaiti hivyo ukiwa na dish la ZUKU mambo safiiiiii

Comments