Jopo la wasanii mahiri leo limefika Ikulu kumshukuru Rais kwa mambo mengi ambayo amewafanyia wasanii katika mwaka huu unaoisha. Katika msafara huo, wanamuziki walitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais kwa kuwapa tuzo za heshima wasanii wakati wa sherehe za miaka 51 ya Uhuru. Wasanii pia walichukua nafasi hiyo kumshukuru Rais kwa kuwajali wakati wa shida kama kuhudhuria misiba, kusaidia wagonjwa na kadhalika.
Wasanii waliokuweko katika msafara huo ni;
Waziri Ally,Abdul Salvador, Cosmas Chidumule, Hamis Mwinjuma (Mwana FA),Hamza Kalala, King Kiki, Ado Mwasongwe, Shakila Said, Simon Mwakifwamba, Carola Kinasha, Ruge Mtahaba, Chiki Mchoma.
Baada ya mazungumzo hayo Rais alitamka kuwa kamati iliyokwenda kumtembelea anategemea itakuwa ndio kiungo kati yake na wasanii wengine. Ili kuweza kufanikisha hilo, wasanii mara moja wameanza mikakati na kuwa na mkutano wa masaa kadhaa kupanga mkakati wa kupata maoni kuhusu maboresho ya urasimishaji wa sekta kutoka kwa wasanii wengi kadri itakavyowezekana. Kamati ya watu watano akiwemo Simon Mwakifwamba, John Kitime, Abdul Salvador, Waziri Ally, Mjumbe kutoka TUMA. Ambao wanatakiwa kuja na taratibu za kuwezesha kufanikiwa kwa zoezi hilo la kukusanya maoni katika kipindi cha siku 7
Comments