MBUNGE
wa Viti Maalumu wa Chama cha Mapinduzi, mkoa wa Iringa, Ritha Kabati,
ameshirikiana na washindi 20 wa ‘Kabati Katiba Star Search’ kutoa kibao kipya
cha Muziki wa Bongo Flava kiitwacho ‘Iringa Bila Ukimwi Inawezakana’, .
Kibao
hicho alichorekodi na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya walioibuka
washindi wa shindano hilo la kusaka vipaji, umerekodiwa katika studio za Top
Magic Sound chini ya mtayarishaji wake mahiri Ecko
Wimbo
huo ni harakati za Mheshimiwa Mbunge Kabati alizozianzisha katika kuwakomboa vijana katika
majanga na makundi hatarishi kama ya uvutaji wa bangi, ngono zembe
zinazochangia maambukizi ya ukimwi – ugonjwa ambao kwa mujibu wa takwimu za
mkoa huu unaongoza kwa maambukizi mapya.
Akiuzungumzia
wimbo huo,Mh. Kabati amesema ana imani ujumbe uliomo utaifanya jamii kubadilika na
hatimae kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi mkoani iringa na
taifa kwa ukjumla.
WIMBO-IRINGA
BILA UKIMWI INAWEZEKANA
ARTIST-KABATI
ALL STARS
STUDIO-TOP
MAGIC SOUND IRINGA
PRODUCER-ECKO
Comments