MSIKIE MWANAMUZIKI AKIKIRI KUWA NI MSHIRIKINA

Katika maisha yangu ya muziki, nimesikia mengi kuhusu wanamuziki kufanya mambo ya kishirikina, lakini kila mara yamekuwa ya 'kusikia tu', si kawaida kumsikia mwanamuziki akijitokeza hadharani kuwa anashiriki katika mambo hayo. Kwa sababu moja au nyingine kuna wanamuziki hujitokeza kujizolea sifa na hata kuogopwa na wenzao kwa ushirikina. Katika siku za karibuni hadithi hizi zimepunguka sana labda kwa kuwa washiriki katika muziki wamezaliwa katika ulimwengu wa kisayansi zaidi, lakini ni wazi tatizo bado liko, nikikumbuka kuwa mwaka jana nilipata taarifa ya mwanamuziki maarufu kufumaniwa makaburini alfajiri na watoto wa kihuni waliomlazimisha awalipe laki moja wasimpeleke serikali za mitaa, na baada ya kumsikiliza na kumuona  huyu dada akihojiwa ITV karibuni, ni wazi bado swala la ushirikina ni kubwa katika maisha ya wanamuziki wengine hebu msikilize hapa chini

Comments