Siku hizi imeanza kuwa kawaida wasanii nchini kuitwa au
kujiita ‘Legends’. Je, neno hili maana yake nini? Neno hili limetokana na neno
la Kilatini ‘legenda’
ambalo maana yake ni ‘Mambo muhimu ya kusomwa’. Hapo awali mambo hayo yalikuwa
ni hadithi na vitendo vya binadamu, vya kusikia, kuhisi na hata kutungwa ambavyo vilionekana
vilifanywa katika historia ya ulimwengu. Katika ‘legends’ kulikuweko na aina ya
ushahidi unaoweza kutetea maelezo husika.
Katika siku za
karibuni, mtu ambaye ameweza kuleta mapinduzi katika fani husika pia ameweza
kuitwa ‘Legend’, kwa mfano Steve Jobs aliyeweza kuleta mabadiliko na mapinduzi
makubwa katika teknolojia iliyotuletea
iPad, iMac, iPhone na kadhalika. Ni kitu kinachochekesha
wakati msanii wa Bongo aliyebobea kwa kurudia mitindo na Beat walioanzisha
wenzie( Congo, Nigeria, South Africa), eti nae anatangazwa kwenye vyombo vya
habari kuwa ni ‘legend’ au pengine kwa ajili ya umri wake tu kuwa mkubwa
tunaambiwa ni ‘legend’. Hi si sawa, ‘ulegend’ unatokana na mambo anayofanya mtu
yanayoleta mchango au mabadiliko katika historia ya fani ya muhusika.
Comments