JE WEWE NI DIVA?


Awali ili kuitwa  Diva ilikuwa lazima mtu awe mwanamke muimbaji maarufu na mwenye ‘outstanding talent’, na tena awe katika muziki wa Opera, huu ni aina ya muziki unaoambatana na mchezo wa kuigiza jukwaani, kwa siku  hizi sifa hii pia wameanza kupewa wanawake maarufu katika filamu, michezo ya kuigiza na muziki. Neno Diva liliingia katika lugha ya Kiingereza katika karne ya 19, likitokana na neno la Kitaliana lililomaananisha Mungu wa Kike. Kwa vyovyote vile Diva lazima awe mwanamke maarufu katika filamu au muziki. Na sifa hii ni ya kupewa na si kujipa, ila kwa vile tuko Kibongobongo usishangae mama ntilie nae akajiita DIVA

Comments