HONGERA WATOTO KWA KAZI NZURI YA SANAA

















Katika vitu vinavyofurahisha ni kukuta watoto wakifanya sanaa kwa ubora wa hali ya juu sana, kwa sisi wasanii wa  zamani unaweza ukajikuta unatumia masaa hata kumi kufaidi kazi hizi. Nimepata bahati ya kuwaona watoto wadogo wakifanya sarakasi, kuimba, kupiga ngoma kwa umahiri wa hali ya juu sana na kupata faraja ya moyo kuwa watu wa kuendeleza gurudumu la sanaa pamoja na mazingira kuwa magumu bado wapo sana. Pata picha za kazi za watoto hawa waliokuwa wakifanya maonyesho kwenye Jumba la Makumbusho katikati ya Dar es Salaam. NAJIULIZA TU KICHWANI WALE WAFADHILI WA SANAA ZA WASANII WAKO WAPI? AU KAZI HIZI HAZILIPI KIBIASHARA NDIO MAANA HAWAKO?

Comments