Kora All Africa Music Awards 2012 hatimae zimefika. Nimeona
niandike kidogo kuhusu hili kwani safari hii wasanii watatu toka Tanzania
wameteuliwa kushiriki katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo nao ni Saida Karoli, Ally Kiba, na Dogo Aslay ambaye kwa
sababu ambazo sijazijua ametajwa kama mshiriki kutoka Kenya. Tuzo za mwaka huu
ziko katika makundi 21, wasanii wa Tanzania watashindana katika makundi matatu
kama ilivyo hapo chini;
1.
Best Male Newcomer of the African continent-
ambapo Dogo Aslay na wimbo wake Niwe
nawe, atapambana na wasanii wengine watano, Floby
wa Burkina Faso, Aziz Azion
wa Uganda, John Chiti wa Zambia, Loyiso wa Afrika ya Kusini na Davido
wa Nigeria.
2.
Best Male Artist of East Africa- katika kundi
hili ndipo Ally Kiba anagombea
tuzo huo kwa wimbo wake Single Boy ambao alimshirikisha Lady Jay Dee, wengine
waliomo katika kinyang’anyiro hicho ni Jimmie
Gait wa Kenya,Chris D wa
Burundi, Kidum wa Burundi, Redsan wa Kenya na Mulatu Astatke wa Ethiopia
3.
Best Female Artist of East Africa- ndilo kundi
tunalomkuta Saida Karoli akigombea
kinyang’anyiro hicho na wimbo wake
wa Sakina, washindani wengine ni Juliana
Kanyomozi wa Uganda, Helen Berhe
wa Ethiopia, Marya wa Kenya, Asther Aweke wa Ethiopia na Ikraan Caraale wa Somalia
Dogo Aslay |
Ally Kiba |
Saida Karoli |
Tuzo za
Kora zilianza kwa mara ya kwanza
1994, zikiwa wazo la mfanya biashara Ernest Coovi Adjovi, mzaliwa wa Benin. Kwa
mara ya kwanza Tuzo sherehe za tuzo hizi zilianza kufanyika nchini Afrika ya Kusini, na kwa miaka ya
kwanza zilikuwa na mgogoro kutokana na kuwa na washindi wa kwanza wote kutoka nchi
zinazozungumza Kifaransa tu, na kwa mara ya kwanza mshindi alipotoka nchi
zinazozungumza Kiingereza wale wanamuziki kutoka nchi zinazozungumza Kifaransa
wakatishia kutoshiriki Tuzo hizo. Pamoja na migogoro yote hiyo ya kukua, KORA
Awards zimekuwa kama Grammy Awards kwa nchi za Afrika na Diaspora yake.
Mwaka huu
kaulimbiu ya Tuzo hizi ni Amani Afrika, na shughuli nzima itafanyika katika
hoteli moja kubwa sana iliyoko Abidjan Ivory Coast. Palais des Congres de l’Hotel
Ivore siku ya Desember 2012.
Comments