UNAMKUMBUKA MWANADADA RAPPER WA MWANZA RAH P ?

 

Rah P alizaliwa Mwanza tarehe 28 June 1986, alikulia Mwanza na kusoma hadi form 6, lakini muda wote mzuka wa Hiphop ukawa umeshamshika japo wazazi wake kwa kweli hawakupendelea yeye afanye shughuli hiyo. Upenzi huo wa fani ya muziki ulimuwezesha kupata kazi ya kuendesha kipindi cha 'African Beat' katika radio ya Kiss 89.8 Fm. 
Mwaka 2004 January ndipo alipoweza kuingia Bongo Records ikiwa chini ya producer P Funk na kurekodi kibao kilichompa sifa 'Hayakuhusu', wakati wa utengenezaji wa video ya wimbo huu, minong’ono ya Rah P kuwa na uhusiano na Mwisho Mwampamba ikaenea, wakati huo Mwisho alikuwa katika ndoa na Ray C.  Rah P kila mara alikuwa akieleza kuwa walikuwa ni marafiki wa kawaida tu na hata Ray C alilijua hilo.
 Baadhi ya nyimbo alizozitoa wakati huo zilikuwa ni Ma Fans, Loony Love na Boys. Kwa muda mwingi sana alikuwa akifanya show zake Uganda maana hata kusoma aliwahi kusoma huko.
Hatimae Rah P alifanya uamuzi wa kuondoka nchini na kuelekea Marekani  kujaribu  kutimiza ndoto yake ya kuwa rapper mkubwa. Alipofika huko mambo hayakuwa kama alivyopanga, alianza shule lakini msaada wa kifedha kutoka nyumbani haukuweko, hivyo katika kuzunguka akakutana na mwanaume waliependana, ambaye alimuahidi angemlipia kukamilisha shule, haikuwa hivyo akajikuta amekwisha zaa mtoto wa kwanza mtu huyo, a hakukuwa tena na swala la shule, kwani mtu huyo akaanza kumnyanyasa mno, hatimae akazaa mtoto wa pili, na mtu huyo akaja kukamatwa kwani alikuwa msambazaji wa madawa ya kulevya, akajikuta peke yake na watoto katika nchi ambayo sheria ilikuwa haimruhusu kufanya kazi… msikilize Rah P mwenyewe akihadithia habari yake ya kusikitisha katika video hii ambayo imetokana na mazungumzo aliyoyatoa kwa KALI TV ONLINE

Comments