The AY, mmoja katika waliopata tuzo za 9th Annual Channel O Music Video Awards


Shamra shamra za 9th Annual Channel O Music Video Awards, zimeweza kuteremsha washindi 14 katika mtanange huu ambao wanamuziki vijana Afrika nzima wamekuwa wakiufuatilia, kwa kujua nani atashinda na pia kwa kuwapigia kura wasanii waliotaka washinde.
D'Banj
Tuzo iliyokuwa kubwa na iliyokuwa kivutio kwa wengi ilikuwa  Most Gifted Video of the Year  ambayo kwa mwaka huu imekwenda kwa  D’Banj kwa video yake ya “Oliver Twist”.
 Zahara, ndiye aliyechukua tuzo la Most Gifted Female Video ambayo aliipata kwa single yake ya  “Loliwe”. Tuzo nyingine ilikuwa kwa ajili ya Most Gifted Newcomer, iliyochukuliwa na Mnaijeria Davido kwa video yake ya “Dami Duro”.
AY
Wanaijeria wengine P Square, wamechukua tuzo ya Most Gifted Duo, Group or Featuring Video kwa video yao ya “Chop My Money” waliomshirikisha Akon na May D. Msouth Afrika DJ Cleo kachukua tuzo la Most Gifted Dance Video kwa video yake ya “Facebook”
Video ya kolabo ya Mzimbabwe Buffalo Souljah na Muangola Cabo Snoop “Styra Inonyengesa” ilichukua tuzo la Most Gifted Ragga Dancehall Video, Mnaijeria mwingine Brymo kachukua tuzo ya Most Gifted Afro Pop Video kwa wimbo wa “Ara
Tuzo la Most Gifted Kwaito Video ilikwenda kwa EES ft Mandoza kwa wimbo wa “Ayoba” , wimbo wa “Oyi” wa Flavour ft Tiwa Savage ndio uliochukua tuzo la Most Gifted R&B Video. Video ya Most Gifted Hip Hop Video imeenda kwa Ice Prince kwa wimbo wake “Superstar”.
P Square
Katika makundi ya maeneo, video ya  Cashtime Fam ya “Shut It Down (Stundee)”, ilichukua tuzo la Most Gifted South Video, wasanii wa Ghana and Nigeria D-Black ft Mo Cheddah kwa video yao ya “Falling” walichukua tuzo la Most Gifted African West Video na  Mtanzania mwenzetu  AY ft Sauti Sol kwa video yao ya  “I Don’t Want to Be Alone” wamechukua tuzo la Most Gifted African East award.
Mwanamuziki mwenye vipaji vingi kutoka South Africa, Oskido, ndie aliyechukua tuzo la heshima la tuzo hizi mwaka  huu


Comments